• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM

Upekee wa kabati la Mswahili

NA KALUME KAZUNGU MSWAHILI asili yake ni Pwani. Huyu ni mja aliyefungamana na tamaduni za kipwani ambazo sanasana ni Uislamu na tamaduni za Kiarabu na Kiajemi, ambaye pia lugha yake mama ni Kiswahili. Aghalabu Mswahili hutumia lugha ya Kiswahili kama kielezeo cha utamaduni wake. Kimsingi, Mswahili pia anaweza kuelezwa kama mtu mahuruti-yaani ni mtu chotara […]

NYS: Waliofungiwa nje kwa sababu ya tattoo waelezea majuto yao

NA MWANGI MUIRURI BAADHI ya vijana waliofika katika vituo vya usajili wa makurutu wa kujiunga na Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) walipigwa na butwaa baada ya kutemwa nje kwa kuwa na michoro ya chale almaarufu ‘tattoo’. Taifa Leo iliwahoji baadhi yao, wakijutia uamuzi waliosema ulitokana na msukumo wa ujana licha ya kukanywa na […]

Waumini waandamana kumtimua pasta ‘anayeanika’ siri za ndoa zao

OSCAR KAKAI NA LABAAN SHABAAN HALI ya Kisirani Kanisani ilishuhudiwa katika kanisa la Redeemed Gospel Church, Chepareria, Kaunti ya Pokot Magharibi. Siku ya ibada Jumapili, washirika walijitenga na shughuli za kanisa na kuandamana dhidi ya Mchungaji wao Timothy Siamoi. Waumini hawa waliojawa na mori walisema mchungaji wao ameshindwa kuwachunga wanakondoo akiishia kuanika hata siri za […]

Mombasa yameremeta Krismasi ikibisha hodi

NA CHARLES ONGADI SHAMRASHAMRA za Sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya zinaendelea kunoga Mombasa huku barabara nyingi katikati mwa jiji zikimeremeta kwa aina mbalimbali ya mapambo. Katika mzunguko wa Makupa katika barabara ilelekeayo kitovuni mwa jiji la Mombasa, kuna aina tofauti ya sanamu za wanyama wa porini waliopambwa kwa taa zenye rangi tofauti zinazomeremeta na […]

Wageni wataabika kupata vyumba vya kulala kipindi kizima cha tamasha za utamaduni Lamu

NA KALUME KAZUNGU UHABA mkubwa wa vyumba vya kulala unashuhudiwa kisiwani Lamu wakati ambapo makala ya 21 ya Tamasha za Utamaduni wa Lamu yanafikia ukingoni. Tamasha hizo za siku tatu zimekuwa zikiendelea tangu Alhamisi na sherehe hizo zinatarajiwa kukamilika Jumamosi usiku. Zaidi ya wageni na watalii 30,000 wamekongamana kwenye mji huo wa kale wa Lamu […]

Harusi hatuna: Jinsi gharama imeingiza baridi wapenzi waliotaka kufunga harusi 2023

NA WINNIE ONYANDO GHARAMA ya maisha inapoendelea kupanda, wapenzi wanaopanga harusi sasa wamebaki njia panda kwani bei za bidhaa mbalimbali zimepanda maradufu. Harusi huhitaji huduma mbalimbali, na kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, baadhi ya wapenzi sasa wanahepa kuandaa harusi ya kukata na shoka kama njia ya kuhifadhi pesa. Maandalizi ya harusi yanahusisha huduma […]

Farasi wanaokula biskuti na kaimati kabla ya kula nyasi

NA FRIDAH OKACHI MFUGAJI wa farasi Mohamed Wangusi mjini Bungoma, anamiliki farasi watatu waliokuwa wakitumiwa na Malkia Elizabeth. Farasi hao wanatumika kwenye mapambo ya harusi na sherehe za kuzaliwa pamoja na kuvuta gari la jeneza nchini Kenya. Malipo kwenye biashara hiyo ikiwa ni Sh1.2 milioni kwa kila sherehe. Mwazilishi huyo wa Royal queens carriage, aliambia Taifa Leo aliuziwa farasi […]

Ugaidi: Familia yataka jamaa arudishwe nchini

BRIAN OCHARO NA FARHIYA HUSSEIN FAMILIA ya mwanamume Mkenya anayezuiliwa Somalia kwa madai ya kusafirishia kundi la kigaidi la al-Shabaab silaha, inataka serikali ya Kenya imrudishe nchini ili ashtakiwe huku. Zakariya Kamal Sufi Abashiekh, 28, alikuwa amekamatwa nchini Aprili kwa madai ya kusaidia Al-Shabaab nchini Somalia kupata silaha kutoka China. Wiki iliyopita, aligonga vichwa vya […]

Fahamu tamaduni za jamii ya Wanubi

NA FARHIYA HUSSEIN KATIKA eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa, sauti zinasikika za watu wakipiga vigelegele, makofi na kuimba nyimbo za sifa. “Tausi huyo, ndege wa angani, tausi ni ndege, mwenye pambo na manyoa,” sauti za wanawake zinasikika kwa umbali. “Mna bahati kushuhudia mojawapo ya harusi za Wanubi,” Bi Halima Abdulrahman akasema mapema Agosti 2023 […]

SIKU YA KISWAHILI DUNIANI: Sherehe kufana miji ya ndani na nje ya Kenya

Na CHRIS ADUNGO KILELE cha maadhimisho ya pili ya Siku ya Kiswahili Duniani (SIKIDU) kitashuhudiwa leo Ijumaa jijini Nairobi na Mombasa, wadau watakapodhihirisha lugha hii ilivyo sehemu muhimu ya tamaduni na taratibu za maisha ya kila siku ya Waswahili – asili, wazawa na waridhiwa wanaoelewana kilahaja. “Maadhimisho haya yatatoa fursa kwa wapenzi wa lugha kujadiliana […]